Powered By Blogger

Thursday, April 28, 2011

NAMNA PRINCE WILLIUM ALIVYOKUTANA NA MCHUMBAKE KATE MIDDLETON

Wapendanao wakitabasamu kwa bashasha kabisa
Watazamaji wakishuhudia harusi ya Mwanamfalme Wiliam na Kate kwa nje kupitia luninga katika kiunga cha Trafalgar Square 
Wakitabasamu kwa hamu na jamu kufu hawa
Prince William na Kate Middleton ndani ya gari la kifahari wakielekea kufunga pingu za maisha katika kanisa maarufu la Westminster Abbey
    Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza Prince Willium amekuwa katika uchumba na mke wake mtarajiwa Kate Middleton a.k.a Ms Shyness kwa takribani miaka saba sasa.
    Wawili hao ambao wanatarajiwa kufunga pingu za maisha mnamo tarehe 29, Aprili, 2011 katika Kanisa kubwa na maarufu jijini London la Westminster Abbey ambapo Askofu Mkuu wa Canterbury Dr. Rowan Willium ndiye atakayewafungisha pingu wanaharusi hao na kati ya wageni maalum waalikwa 1900 ni aliyekuwa Mchezaji soka maarufu wa Manchester Utd na timu ya taifa ya England David Beckham atakayeambatana na Mkewe Victoria Beckham, Mwanamuziki na mmoja wa Marafiki wakubwa wa Marehemu Princess Diana ( aliyefariki kwa ajali ya gari huko Paris mwaka 1997) ambaye ni Mama Mzazi wa Prince Willium, Sir Elton John, Waziri Mkuu wa nchi hiyo David Cameron na Mwanamuziki wa hip hop kutoka Marekani Kanye West, Rowan Atkinson ( Mr. Bean) ambaye atatumbuiza pamoja na Sir John, Rais Obama  pamoja na Mawaziri Wakuu wa zamani wa nchi hiyo Gordon Brown na Tony Blair hawakutajwa katika idadi hiyo ya Wageni Maalum. Mbali na hao pia kutakuwa na Viongozi zaidi ya 50 kutoka nchi mbalimbali.
     Harusi hiyo amabayo inatarajiwa kutazamwa na watu zaidi ya bilioni 2 kupitia luninga na mtandao wa Youtube duniani kote, isitoshe kutakuwapo na luninga litakaloonyesha harusi hiyo moja kwa moja katika viunga vya Trafalgar Square na Hyde Park, ambapo wakazi wa London na miji mbalimbali ya karibu watashuhudio tukio hilo maarufu katika historia ya Familia ya Malkia na Dunia kijumla. harusi hiyo inakadiriwa kugharimu zaidi ya pauni milioni 20 za kiingereza.
     Akimuelezea Mchumba wake Kate ambaye atavishwa pete ya Marehemu Princess Diana,  Prince anadai kuwa ni mpenda utani na humfurahisha sana kwani yeye hakujaaaliwa hulka hiyo. Kate anasema kuwa angependa harusi yao ifanyike haraka iwezekanavyo "Nilifurahi sana siku nilipojuana na Prince" alinukuliwa akisema hivyo. Inasemekana kuwa Kate alishawahi kuwa na picha ya utoto ya Prince katika chumba chake aliposailiwa kuhusu hili hakukaukiwa maneno "Nilikuwa na picha ya  mtoto alevaa dengrizi ya Levis na sio Willim" alijibu madai hayo, naye Willium alimjibu kwa ksema " Ni mimi ndiye nilivaa Levis"
    Prince alikutana na Kate katika Chuo Kikuu cha St. Andrews ambapo wote walikuwa wakisoma somo la Historia "Tulikuwa tukicheka pamoja na wote tulitokea kupendelea vitu vinvyofanana" alinukuliwa na watu wake wa karibu. Walitangaza uchuimba wao tarehe 16, Nov , 2010 huko Kenya walipokuwa katika matembezi ya siku 10 kwenye mbuga ya  Lewa Wildlife Conservancy wakati Prince akisherehekea kufuzu kwake mafunzo ya urubani wa ndege za kijeshi (R.A.F)
    Prince Willium alizaliwa June 21, 1982, St. Mary Hospital, London naye Kate Middleton anayetoka familia ya tabaka la kati alizaliwa Jan 9, 1982 huko Reading, Berkshire na shahada ya uzamili katika sanaa na historia.


        "The only way to have a friend is to be One"
                                                                       -Emerson

Friday, April 22, 2011

CHANGAMOTO KWA VIONGOZI WA KIAFRIKA

         Katika kampeni zake za kuwania Uwaziri Mkuu, David Cameron, Msomi wa Siasa, Falsafa na Uchumi kutoka Chuo Kikuu Maarufu na Aghali Duniani cha Oxford alikuwa na sera thabiti za kuziendeleza taifa lake na wananchi wenzake ambapo katika kampeni zake alizikatia kaulimbiu ya "BIG SOCIETY" ambayo ni kama Flagship ambapo katika motto wake huo aliunakshi nakshi na mikakati madhubuti kama ifuatayo;

(a)Give societies more powers, localism&devolution.
(b)Encourage people to take active role in their communities, volunteerism.
(c)Transfer power from Central Govt to Local Govt.
(d)Support co-ops, mutual, charities, and social enterprises.
(e)Publish govt data (open/transparent govt) means to exists to generate develop and showcase new ideas to help people to come together in their neighbourhoodsto do good things.

       Ukitathmini kwa umakini, kwa mawazo kuntu na yasiyo na mgando harakati za bwana David dhidi ya nchi yake utagundua kuwa Wazungu na Waafrika wana tofauti katika uratibu, utendaji na utekelezaji wa mambo mbalimbali kama huamini fikiria kuwa ni kiongozi gani umewahi kumsikia katika kampeni zake akiwa na mawazo, fikra na mipango endelevu kwa wananchi wake? Hili la Cameron ni moja, mbili na tatu unayo wewe Mpenzi Msomaji...
     
       Nashindwa kumalizia makala hii bila kukuchopolea moja ya nukuu zake alizowahi kuongea katika kampeni zake ambazo zilikuja kumuweka kileleni hapa alipo sasa, alisema hivi...

                                "I got into politics because i love this country (Great Britain)"
                                                           David Cameron, Waziri Mkuu wa Uingereza.

Saturday, April 16, 2011

MTOTO WA CHINA ATEULIWA KUWA BALOZI WA MAPINDUZI YA KIJANI WA UMOJA WA MATAIFA

Mtoto Li Hongyan akifurahia uteuzi wake kama Balozi mdogo kuliko wote wa Mapinduzi ya Kijani Duniani huko katika Makao Makuu ya UN Habitat, jijini New York, Marekani
  

    Li Hongyan binti kutoka nchini China ameteuliwa kuwa Balozi wa Umoja huo wenye nchi wanachama wengi kuliko yote duniani katika harakati zake za kutunza mazingira ( Green Revolution).
    Li 7, ambaye ndio amewahi kuwa mwakilishi mdogo kuliko wote katika historia ya Umoja huo. Anahamasisha jamii inayomzunguka kwa kuhodhi mapinduzi hayo muhimu kwa mintaarafu ya kuilinda dunia yetu dhidi ya majanga.
    Akiongea baada ya kupokea wadhifa huo wa heshima Li anadai kuwa angependa kuwafundisha wanafunzi wenzie maarifa hayo ili wapita njia wapate kushangaa pindi wapitapo karibu na mazingira hayo.
    Naye Rais wa Uga huo wa sita amesifia sana juhudi za Wachina kuhamasisha watoto wao dhidi ya utunzaji wa mazingira . Anaamini kuwa vitendo vya mtoto kama Li vitahamasisha watoto wengine kupigania mapinduzi hayo,
 
    Je, wako wapi watoto kama akina Li kutoka bara Afrika?

    "Nyota njema huonekana asubuhi"
                                   Msemo wa Kisuaheli

Friday, April 15, 2011

UINGEREZA YAZIDI KUKITA SENYENGE DHIDI YA WAHAMIAJI

Waziri Mkuu wa Uingereza na Kiongozi wa Chama cha Conservative David Cameron
     Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kutoka chama cha mahafidhina (Conservative) amesema kuwa nchi yake inapanga mikakati thabiti ya kupunguza wimbi la wahamiaji wanaotoka nje ya eneo la uchumi wa ulaya, akiongelea masharti hayo kupitia luninga la BBC amedai kuwa Uingereza imefikia hatua ya kupunguza wahamiaji kutoka mamia mpaka makumi japokuwa anajua hasa umuhimu wao, ukienda shuleni utawakuta walimu kutoka Uganda, hospitalini utawakuta waganga mashuhuri kabisa kutoka India na Pakistan na bado ukipita mitaa na ofisi  mbalimbali nchini hapo utakutana na raia wengi kutoka nchi za jumuiya ya madola (Commonwealth) wakifanya shughuli tofauti zinazoendeleza Taifa hilo lenye takribani ya idadi ya watu milioni 60. David Cameron ametoa sababu kuwa ni pamoja na kuondoa mpango wa fedha za ruzuku (Employment Benefits) kwa watu wasio na ajira hasa wahamiaji ambalo amesisitizia kuwa huwafanya wenyeji (Waingereza) wabweteke na wasubirie hiyo fadhila.
     Kwa upande wa siasa amedai kuwa wahamiaji wengi hawajui mfumo wa kisiasa wa nchini hapo, na kufanya washindwe kufikia malengo yao kama Tories, katika upande wa elimu bwana Cameron amedai kuwa serikali yake ikiungana pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu watakuwa makini kwa kuruhusu wanafunzi waliofaulu zaidi kutoka nje ya nchi yake kujiunga na Vyuo mbalimbali nchini. Amepiga kengele kuwa ni lazima kila mhamiaji kukimanya kingereza kwa ufasaha.
     Takwimu za  Uhamiaji UK zinadai kuwa kumekuwa na ongezeko la wahamiaji zaidi ya Mil 2.2 toka mwaka 1997-2009, Japokuwa Chama cha Lib Dems kimeyapinga madai hayo kwa kusema kuwa uhamiaji ni muhimu sana katika kupiga kura. Naye Mchambuzi wa siasa za Uingereza wa Idhaa ya Kiswahili wa BBC Suleiman Salum alipokuwa akihojiwa na Idhaa hiyo amedai kuwa masharti hayo ni ya kibaguzi na hayana tija na akaendelea kuhoji kuwa "Kitu gani kinafanya Kiingereza Uingereza?"
     Hizi ni changamoto nyingine kwa Raia wasio Wazungu...

Chanzo : Idhaa ya Kiswahili ya BBC

David Cameron's immigration speech