Powered By Blogger

Thursday, February 17, 2011

MABOMU BILA VITA MAANA YAKE NINI?

Bomu likiwa limezagaa katika moja ya njia za huko Gongo la Mboto ambapo milipuko yake iligharimu maisha ya watu na kujeruhi mamia wao
  Usiku wa kuamkia Alhamisi Mji wa Dar-Es-Salaam ulipatwa na dhoruba kubwa ya ulipukaji ovyo wa mabomu katika mitaa ya Gongo La Mboto ambapo dhahama hiyo ilianza majira ya saa mbili usiku. Taarifa kutoka baadhi ya vituo mbalimbali vya habari nchini vinadai kuwa tsunami hilo limegharimu baadhi ya maisha ya watu na kujeruhi mamia wao ambao wengi wao walikimbizwa katika Hospitali ya Amana na wengine Muhimbili baada ya kuonekana kudhuriwa zaidi janga hilo, wengine wakipotezana na familia zao kutokana na harakati za kujikomboa na gharika hilo ambalo ni mara ya pili kulimbuka Taifa hili linalosifika kwa Amani na Utulivu Duniani kote.
 Swali la kujiuliza ni kwamba nani atalipa Damu za Marehemu ambao idadi yao haijapatikana mpaka wakati huu nikiichonga kalamu hii katika tarakilishi?