Powered By Blogger

Wednesday, August 17, 2011

VURUGU ZA UK ZAWEZA KUTOKEA HATA KWA KOLONI LAKE LA TANZANIA

Marehemu Mark Duggan siku tano kabla ya kifo chake
     Vurugu za hivi karibuni nchini Uingereza zimejaribu kufumbua walimwengu macho kuwa dunia ni moja, tabu na raha machungu na matamu, hisia na fikra zile zile, mahitaji na matumizi ni yale yale katika dunia hii tofauti ni chache sana kama mifumo ya elimu, mbari, teknolojia n.k

     Tafrani hizo zinaturudisha nyuma kidogo tangu miaka ya ya 1980's ambapo vitongoji kadhaa vya Brixton na Tottenham jijini London vilishawahi kukumbwa na sekeseke la hivi majuzi na kuuawa kwa askari , na kuharibika kwa mali na baadhi ya watu kuuwawa hivo ya juzi ilikuwa ni muendelezo tu wa historia hiyo ya nyuma kwa ni tabia ni kama ngozi huwezi kuibadili.

     Siku ya alhamisi ya tarehe 4,agosti katika kitongoji cha Tottenham ambacho wenyeji wake wengi ni waafrika kutoka visiwa vya karibiani wajamaika, wagaiana, wababadosi, wa senti lushia n.k aliuawa kwa kupigwa risasi na makachero wa Scotland Yard kijana mweusi mwenye miaka 29 Mark Duggan ambaye ni dereva wa taksi aliyeshukiwa kutaka kuwapiga polisi risasi na anayejishughulisha na biashara haramu za madaya ya kulevya na uuzaji silaha katika jiji hilo lenye zaidi ya watu milioni 10 na lugha zaidi ya 300 za nchi mbalimbali zinazozungumzwa na wakazi wa hapo.

     Kisa hiki mkafiri kikasababisha kulipuka kwa vujo za vijana wa hapo waliokuwa wakidai sababu ya kuuawa kwa mwenzao, na ndipo majibu yaliposhindwa kuwaridhisha wakaona suluhisho ni kuingia mitaani na kufanya vurugu ambapo zimesababisha baadhi ya watu kukosa makazi, biashara na hata magari kwani walikuwa wakipora ( LOOTING) maduka makubwa na kuyachoma moto na hata kusimamisha mabasi ya gorofa mekundu ya umma yanayobeba taswira ya usafiri wa jiji la London.

    Ubaradhuli huo haukuishia tu London, bali ulianza kusambaa miji mingine kama Birmingham, Liverpool, Manchester, Wolverhampton na Nottingham, huku ikidaiwa kuwa vijana hao waliweza kufanya vujo hizo kwa kutumiana jumbe kupitia mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook kutaarifiana mahali ambapo walitaka kwanda kupora.

Kufuatia vurugu hizo Waziri Mkuu wa nchi hiyo David Cameron hakuwa na budi kukatisha safari yake ya mapumziko nchini Italy na kurejea nchini mwake na kuitisha kikao cha kujadili masuala makini sana ( COBRA MEETING) na kuota agizo kuongezwa kwa askari wa usalama kuanzia 6000 hadi 16000, ambao wameweza kusitisha fujo hizo zilizodumu kwa takribani siku nne mfululizo na kusababisha uharibifu, mauaji katika miji mbalimbali.

Taarifa kutoka idara ya polisi inadai kuwa zaidi ya watu 3000 ambao zaidi ya 83 ni vijana wenye umri wa miaka zaidi ya 20 ilyobaki ni chini ya miaka 18 wameshakatwa kufuatia vurugu hizo na kesi zao zinasikilizwa mwenye umri mdogo kuliko wote ni mtoto wa miaaka 11 mabaye alionekana kwenye cctv kamera akiiba chupa ya mvinyo katika duka moja jijini London.

      Baadhi ya wataalamu wa masuala ya kijamii, kihistoria na wanaharakati wa watu watu weusi kama Nathan John, Symeon Brown na Darcus Howe wamesema kuwa Tottenham ni sehemu ambayo jamii yake imesahauliwa sana na serikali, ni mahali ambapo kuna maskini wengi weusi na vijana wengi wa hapa hawajui mustakabali wa maisha yao ya baadae, wazazi wao maskini, wanalelewa na mama zao, baba zao wamewakimbia  kutokana na majukumu na matatizo ya kuvunjika kwa ndoa, wamemaliza shule lakini hawana kazi, kifupi ni kama vile familia iliyotelekezwa na wazazi, pia hawana mahusiano mazuri na polisi, vijana wengi husumbuliwa sana na polisi bila sababu, husimamishwa majiani wakapekuliwa, wakangurumiwa na hata kutishiwa, lakini hii yote ni kwa sababu ya umaskini na ubaguzi wa rangi, hivyo tafrani za juzi  ni kama VIRAL VOICE yaani sauti yenye kirusi.

       Funzo ni nini? hapa nyumbani Tanzania kumekuwa na matabaka makubwa sana na sana baina ya walionacho na wasio nacho, kuanzia kwenye elimu, afya, makazi, uchumi, siasa, leo hii mtoto wa mkulima anapewa mkopo sawa na mtoto wa kigogo chuo kikuu, kazi za mashati meupe wanapewa watoto wa wakubwa au nafasi za kazi hutangazwa baada ya kupatikana watu, siasa ya sasa ni ile ya kupigizana makelele yasiyo na tija wala faida kwa mkulima zaidi ya wanasiasa kujizolea umaarufu tu, mishahara ya wafanyakzi wa serikali ni midogo, kodi kubwa, huduma duni za jamii, wanasiasa wanajiongezea posho na marupurupu kila kukicha, mkulima anapangiwa bei ya uzi na serikali, askari polisi hawana ushirikaino na raia, ukiomba kazi rushwa zimetawala, Profesa Chinua Achebe anasema wanaangalia huyu ni nani badala ya anajua nini, kujuana katika kazi na ajira ndipo kasumba iliyojaa hapa nyumbani Tanzania, yako mengi mateso wayapatayo maskini nchi hii inayosifika kwa amani na upendo, inawezekana kuwa na ustawi wa jamii ikiwa ule ubinafsi wa titi la paka tutakapoamua kulikata jamani watanzania, we are equal before the God, why others act as Modern Earthly Gods nowadays?


Kama Uingereza yameweza kutokea hayo yaliyokea kwa ajili ya mfumo kandamizi na usiojali asiyenacho basi hata mataifa ya dunia ya tatu yajiandae kwani siku mjinga akirevuka, basi mjanja yu mashakani.