Powered By Blogger

Friday, April 15, 2011

UINGEREZA YAZIDI KUKITA SENYENGE DHIDI YA WAHAMIAJI

Waziri Mkuu wa Uingereza na Kiongozi wa Chama cha Conservative David Cameron
     Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron kutoka chama cha mahafidhina (Conservative) amesema kuwa nchi yake inapanga mikakati thabiti ya kupunguza wimbi la wahamiaji wanaotoka nje ya eneo la uchumi wa ulaya, akiongelea masharti hayo kupitia luninga la BBC amedai kuwa Uingereza imefikia hatua ya kupunguza wahamiaji kutoka mamia mpaka makumi japokuwa anajua hasa umuhimu wao, ukienda shuleni utawakuta walimu kutoka Uganda, hospitalini utawakuta waganga mashuhuri kabisa kutoka India na Pakistan na bado ukipita mitaa na ofisi  mbalimbali nchini hapo utakutana na raia wengi kutoka nchi za jumuiya ya madola (Commonwealth) wakifanya shughuli tofauti zinazoendeleza Taifa hilo lenye takribani ya idadi ya watu milioni 60. David Cameron ametoa sababu kuwa ni pamoja na kuondoa mpango wa fedha za ruzuku (Employment Benefits) kwa watu wasio na ajira hasa wahamiaji ambalo amesisitizia kuwa huwafanya wenyeji (Waingereza) wabweteke na wasubirie hiyo fadhila.
     Kwa upande wa siasa amedai kuwa wahamiaji wengi hawajui mfumo wa kisiasa wa nchini hapo, na kufanya washindwe kufikia malengo yao kama Tories, katika upande wa elimu bwana Cameron amedai kuwa serikali yake ikiungana pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu watakuwa makini kwa kuruhusu wanafunzi waliofaulu zaidi kutoka nje ya nchi yake kujiunga na Vyuo mbalimbali nchini. Amepiga kengele kuwa ni lazima kila mhamiaji kukimanya kingereza kwa ufasaha.
     Takwimu za  Uhamiaji UK zinadai kuwa kumekuwa na ongezeko la wahamiaji zaidi ya Mil 2.2 toka mwaka 1997-2009, Japokuwa Chama cha Lib Dems kimeyapinga madai hayo kwa kusema kuwa uhamiaji ni muhimu sana katika kupiga kura. Naye Mchambuzi wa siasa za Uingereza wa Idhaa ya Kiswahili wa BBC Suleiman Salum alipokuwa akihojiwa na Idhaa hiyo amedai kuwa masharti hayo ni ya kibaguzi na hayana tija na akaendelea kuhoji kuwa "Kitu gani kinafanya Kiingereza Uingereza?"
     Hizi ni changamoto nyingine kwa Raia wasio Wazungu...

Chanzo : Idhaa ya Kiswahili ya BBC

David Cameron's immigration speech

1 comment: