Powered By Blogger

Monday, May 16, 2011

YUKO WAPI MADELEINE McCANN WALIMWENGU?

Mtoto Madeleine McCann (pichani chini) alitoweka mchana wa tarehe 3, May, 2007 siku ya Alhamisi katika sikukuu na wazazi wake pamoja na ndugu zake mapacha Sean na Amelie katika Hoteli ya Praia Da Luz katika mkoa wa Alvare huko nchini Ureno.
Alitoweka siku chache baada ya sherehe za kutimiza miaka 4 hakuonekana mpaka leo. Kate na Gerry McCann (wazazi wake) wanasema walimuacha mtoto wao katika chumba cha kulala wakati walipoelekea kula umbali wa mita 120 majira ya saa 2;30 usiku, walirudi saa 4 usiku na Kate kwenda moja kwa moja hadi chumbani na kutomuona Mwanae, alikwisha chukuliwa muda sana na mtu ambaye hajafahamika hadi hivi leo.
Robert Murat, mkazi wa Alvaro alishukiwa kuwa ndiye aliyemchukua mtoto huyo ila ushahidi wa kina ulikosekana na hatimaye akaachiwa July, 21
Sergey Malinke,22 mwenye asili ya Urusi naye pia alihusishwa na tukio hilo na mwishowe akaachwa huru kama Mshukiwa wa awali.
Polisi wa Ureno walienda kaika chumba cha Madeleine na kufanya uchunguzi wa kisayansi wa kumpata mhusika kwa njia ya DNA yaani Forensic Evidence ila zoezi hilo halikufanikiwa pia kwani hawakupata vinasaba vya mtu yoyote mule chumbani.
Wasamaria wema nchini Uingereza walitangaza kila aina ya zawadi kwa yeyote atakayefanikiwa kumpata binti, mfuko wa kuchangisha fedha wa MADELEINE McCANN FUND; LEAVING NO STONE UNTURNED ulianzishwa ili uweze kuchochea watu wasaidiane katika kumsaka Malaika huyo wa Mungu. Jitihada za kumpata Madeleine hazijafanikiwa kuzaa matunda hadi hivi sasa.

                              Mungu amlinde Madeleine McCann popote pale alipo, Amina

1 comment:

  1. Unafikiri atakuwa wapi, kuna watu wamemuuba, au kuna nini kilimpata? Huo ni mtihani, nawapa pole wazazi wake na jamaa, ...nawaombea subira njema, ipo siku watamuona, mungu yupo pamoja nawo!

    ReplyDelete