Hakuna mtu wa kukataa wala kukubali kuwa Mzee huyu aliwanyima sana usingizi Wamarekani kwa zaidi ya muongo, watu walikuwa wakiiishi kwa hofu na wahaka sana kwa sababu yake maskini, hasa baada ya mashambulizi yake katika kituo cha biashara duniani World Trade Centre jijini New York na Kambi za Pentagon katika mji wa Washington ambayo yalipoteza maisha ya watu zaidi ya 3000, miaka 3 kabla alihusishwa pia na milipuko ya mabomu katika Balozi za Marekani mjini Dar-es-Salaam na Nairobi ambapo zaidi ya watu 200 walihofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa, na shambulizi hili ambalo liliendana na oparesheni kali dhidi ya ugaidi na hatimaye kukamatwa kwa baadhi ya washukiwa wa kitanzania ambaye mmojawapo ni Mzanzibar Mohammed Ghailani ambaye alipatikana na hatia na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha maisha Marekani miezi kadhaa mwaka huu maskini, Mohammed angali kijana 23 atasotea maisha yake yote gerezani.
Mmoja wa wachambuzi wa siasa za ulimwengu Suleman Salum alihoji sana kuhusu kifo cha Osama kwa kudai kuwa hata wamarekani ni magaidi kwa namna walivyomuua Osama kwa sababu alipaswa akamatwe apelekwe Mahakamani akatoe sababu kwa nini alikuwa akifanya vitendo hivyo viovu kama cha September 11? lakini kitendo cha wao kumuua kimedhihishia ulimwengu uchakaramu na umuflis wao, lakini pia opereshani za kumsaka mtu huyu pia zilikuwa za kigaidi kwa kuvamia nchi za Afghanistan, Iraq na kuanza kuteketeza mamia ya watu ya watu ambao hawana hatia hata chembe, Salum aliiambia Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
HOJA KUNTU;
Kumekuwa na kasumba ya watu walio na majina ya kiislamu kubaguliwa sana pindi watakapo kusafiri kwenda nchi mbalimbali za Maghreb kama Marekani na Uingereza kwa kuwanyima viza na hata vibali vya kuishi katika nchi hizo kwa ajili ya majina yao, hivi ni kweli jina huweza sadifu itikadi, hulka na mwenendo mzuri au mbaya wa mtu jamani kama si ubaguzi wangapi washafanya matukioya ajabu ilhali si waislamu kama Coperland aliyekuwa akiwaua watu weusi kule kitongocha Brixton kusini mwa London, Uingereza huyu naye ni muislam na ana jina la kiislam kama Osama? Rais wa Marekani Barack Obama amedai kuwa suala la Ugaidi halihusishwi na dini yoyote bali imani za mtu tu, huwezi kumnyooshea mtu kidole kuwa ni gaidi kwa kuwa ni mwislam au mkristo, la hasha, alidai Mjaluo Obama.
Marehemu Osama bin Laden akiwa na Mwandishi wa Habari Hamid Amir mwaka 1997 |
Marehem Osama aliamini kuwa Sharia Law ndo suluhisho la matatizo yote ulimwenguni...
R.I.P
No comments:
Post a Comment