Wapendanao wakitabasamu kwa bashasha kabisa |
Watazamaji wakishuhudia harusi ya Mwanamfalme Wiliam na Kate kwa nje kupitia luninga katika kiunga cha Trafalgar Square |
Wakitabasamu kwa hamu na jamu kufu hawa |
Prince William na Kate Middleton ndani ya gari la kifahari wakielekea kufunga pingu za maisha katika kanisa maarufu la Westminster Abbey |
Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza Prince Willium amekuwa katika uchumba na mke wake mtarajiwa Kate Middleton a.k.a Ms Shyness kwa takribani miaka saba sasa.
Wawili hao ambao wanatarajiwa kufunga pingu za maisha mnamo tarehe 29, Aprili, 2011 katika Kanisa kubwa na maarufu jijini London la Westminster Abbey ambapo Askofu Mkuu wa Canterbury Dr. Rowan Willium ndiye atakayewafungisha pingu wanaharusi hao na kati ya wageni maalum waalikwa 1900 ni aliyekuwa Mchezaji soka maarufu wa Manchester Utd na timu ya taifa ya England David Beckham atakayeambatana na Mkewe Victoria Beckham, Mwanamuziki na mmoja wa Marafiki wakubwa wa Marehemu Princess Diana ( aliyefariki kwa ajali ya gari huko Paris mwaka 1997) ambaye ni Mama Mzazi wa Prince Willium, Sir Elton John, Waziri Mkuu wa nchi hiyo David Cameron na Mwanamuziki wa hip hop kutoka Marekani Kanye West, Rowan Atkinson ( Mr. Bean) ambaye atatumbuiza pamoja na Sir John, Rais Obama pamoja na Mawaziri Wakuu wa zamani wa nchi hiyo Gordon Brown na Tony Blair hawakutajwa katika idadi hiyo ya Wageni Maalum. Mbali na hao pia kutakuwa na Viongozi zaidi ya 50 kutoka nchi mbalimbali.
Harusi hiyo amabayo inatarajiwa kutazamwa na watu zaidi ya bilioni 2 kupitia luninga na mtandao wa Youtube duniani kote, isitoshe kutakuwapo na luninga litakaloonyesha harusi hiyo moja kwa moja katika viunga vya Trafalgar Square na Hyde Park, ambapo wakazi wa London na miji mbalimbali ya karibu watashuhudio tukio hilo maarufu katika historia ya Familia ya Malkia na Dunia kijumla. harusi hiyo inakadiriwa kugharimu zaidi ya pauni milioni 20 za kiingereza.
Akimuelezea Mchumba wake Kate ambaye atavishwa pete ya Marehemu Princess Diana, Prince anadai kuwa ni mpenda utani na humfurahisha sana kwani yeye hakujaaaliwa hulka hiyo. Kate anasema kuwa angependa harusi yao ifanyike haraka iwezekanavyo "Nilifurahi sana siku nilipojuana na Prince" alinukuliwa akisema hivyo. Inasemekana kuwa Kate alishawahi kuwa na picha ya utoto ya Prince katika chumba chake aliposailiwa kuhusu hili hakukaukiwa maneno "Nilikuwa na picha ya mtoto alevaa dengrizi ya Levis na sio Willim" alijibu madai hayo, naye Willium alimjibu kwa ksema " Ni mimi ndiye nilivaa Levis"
Prince alikutana na Kate katika Chuo Kikuu cha St. Andrews ambapo wote walikuwa wakisoma somo la Historia "Tulikuwa tukicheka pamoja na wote tulitokea kupendelea vitu vinvyofanana" alinukuliwa na watu wake wa karibu. Walitangaza uchuimba wao tarehe 16, Nov , 2010 huko Kenya walipokuwa katika matembezi ya siku 10 kwenye mbuga ya Lewa Wildlife Conservancy wakati Prince akisherehekea kufuzu kwake mafunzo ya urubani wa ndege za kijeshi (R.A.F)
Prince Willium alizaliwa June 21, 1982, St. Mary Hospital, London naye Kate Middleton anayetoka familia ya tabaka la kati alizaliwa Jan 9, 1982 huko Reading, Berkshire na shahada ya uzamili katika sanaa na historia.
"The only way to have a friend is to be One"
-Emerson
No comments:
Post a Comment