Powered By Blogger

Wednesday, May 11, 2011

KUMBUKUMBU ZA BOB MARLEY

Marehemu Bob Marley akicharaza gitaa.
Ni mwaka wa 30 tangu Gwiji, mpiganiaji haki na mwanamuziki wa Reggae Bob Marley alipoaga dunia tarehe 11, may, 1981 katika hospitali ya Cedars Lebanon, Miami, Florida, Marekani.

Bob alikuwa mpiga gitaa la ridhimu na muimbaji kiongozi wa bendi za Ska, Rocksteady, Reggae na hatimaye The Wailers (1963-1981), alihamasishwa kuimba  na masuala ya jamii yake katika nchi ya jamaika, kisiasa na kiutamaduni, nyimbo zake kali kama "I shot the Sheriff", "No woman no cry" "Could you be loved" "Jammin na Sti it up" katika albamu alizofanya na kundi la The Wailers za "Buffalo Soldies na Iron Lion Zion". Miaka mitatu baadaye baada ya kifo chake albamu  ya "The Legend'" ilitolewa na kuwa albamu iilouza zaidi ya nakala milioni 25 na kufikia hadhi ya Platinum (Diamond) huko nchini Marekani

Bob Marley alizaliwa kama Nesta Robert Marley katika kijiji cha Nine Mile huko St. Ann Parish na Baba yake Mzee Narval Sinclair Marley ambaye alikuwa mjamaika- mzungu mwenye lafidhi ya Uingereza ambaye familia yake ilitokea Essex, Uingereza na nahodha wa meli ambaye alikuja kumuoa mjamaika-mwafrika Codella Booker aliyekuwa na umri wa miaka 18, walijitahidi kuea familia yao japokuwa Babake Bob muda mwingi alikuwa safarini ambapo mwaka 1955 Bob akiwa na miaka 10 Babake alifariki kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo(Heart attack) akiwa na miaka 60, alipooulizwa kuhusu asili yake Bob alijibu kuwa

            "I dont have prejudice against meself. My father was a white and my mother was black, then call me half-caste or whatever. Me dont dip on nobody's side. Me dont dip on the black man's side nor the white man's side. Me dip on God's side, the one who create me and cause me to come from black and white"

Alipokuwa katika ziara zake za Ulaya , Bob alipata kudhuru kidole chake alipokuwa akicheza mpira wa miguu huko jijini Paris,Ufaransa mwaka 1977 alikutwa na kansa aina ya Acral Lentiginon Melanoma aina ya  Malignant melanoma. Baadaye alirudi Marekani ambapo alifanya maonyesho mawili (Gigs) katika ukumbi wa Madison Square Garden jijini New York huku akijua kuwa kupona yeye ilikuwa haiwezekani maskini. Ugonjwa ulisambaa hadi katika ubongo na hatimaye akapelekwa katika hospitali ya huko Miami ambapo aliaga dunia asubuhi ya May, 11, 1981 na kuzikwa May, 21, mazishi yake yalifanywa kitaifa karibu na mahala alipozaliwa yakihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamaika Edward Seaga ambaye alitoa wasifu ufuatao kwa Marehemu

                "His voice was an omnipresent cry in our electronic world. His sharp features, majestic looks and prancing style a vivid etching on the landscapes of our minds. Bob Marley was never seen. He was an experience which left an indelible in print with each encounter. Such a man can not be erased from the mind. He is part of the collective consciousness of the nation"

alihitimisha Waziri katika msiba wa kinara huyu aliyepigania uhuru, haki na usawa wa watu weusi kupitia nyimbo zake. Mungu amrehemu.....

1 comment:

  1. Sinema mpya kuhusu Bob Marley imetoka mwezi huu tarehe 20 mjini London. Sinema hii (inayoitwa "Marley") iliyokubaliwa na familia yake-inamulika upande wa maisha ya Bob na hisia au tabia zake zisizojulikana. Mathalan alijisikiaje kama chotara- babake Mzungu hakumjali- au kuhusu wanawake na watoto wengi aliokua nao? Soma zaidi hapa:
    http://en.wikipedia.org/wiki/Marley_%28film%29

    ReplyDelete