Waziri Mkuu wa Uingereza na Kiongozi wa Chama cha Conservative David Cameron |
Kwa upande wa siasa amedai kuwa wahamiaji wengi hawajui mfumo wa kisiasa wa nchini hapo, na kufanya washindwe kufikia malengo yao kama Tories, katika upande wa elimu bwana Cameron amedai kuwa serikali yake ikiungana pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu watakuwa makini kwa kuruhusu wanafunzi waliofaulu zaidi kutoka nje ya nchi yake kujiunga na Vyuo mbalimbali nchini. Amepiga kengele kuwa ni lazima kila mhamiaji kukimanya kingereza kwa ufasaha.
Takwimu za Uhamiaji UK zinadai kuwa kumekuwa na ongezeko la wahamiaji zaidi ya Mil 2.2 toka mwaka 1997-2009, Japokuwa Chama cha Lib Dems kimeyapinga madai hayo kwa kusema kuwa uhamiaji ni muhimu sana katika kupiga kura. Naye Mchambuzi wa siasa za Uingereza wa Idhaa ya Kiswahili wa BBC Suleiman Salum alipokuwa akihojiwa na Idhaa hiyo amedai kuwa masharti hayo ni ya kibaguzi na hayana tija na akaendelea kuhoji kuwa "Kitu gani kinafanya Kiingereza Uingereza?"
Hizi ni changamoto nyingine kwa Raia wasio Wazungu...
Chanzo : Idhaa ya Kiswahili ya BBC
Safi sana kijana!!!blog imetulia..
ReplyDelete