Powered By Blogger

Monday, May 16, 2011

YUKO WAPI MADELEINE McCANN WALIMWENGU?

Mtoto Madeleine McCann (pichani chini) alitoweka mchana wa tarehe 3, May, 2007 siku ya Alhamisi katika sikukuu na wazazi wake pamoja na ndugu zake mapacha Sean na Amelie katika Hoteli ya Praia Da Luz katika mkoa wa Alvare huko nchini Ureno.
Alitoweka siku chache baada ya sherehe za kutimiza miaka 4 hakuonekana mpaka leo. Kate na Gerry McCann (wazazi wake) wanasema walimuacha mtoto wao katika chumba cha kulala wakati walipoelekea kula umbali wa mita 120 majira ya saa 2;30 usiku, walirudi saa 4 usiku na Kate kwenda moja kwa moja hadi chumbani na kutomuona Mwanae, alikwisha chukuliwa muda sana na mtu ambaye hajafahamika hadi hivi leo.
Robert Murat, mkazi wa Alvaro alishukiwa kuwa ndiye aliyemchukua mtoto huyo ila ushahidi wa kina ulikosekana na hatimaye akaachiwa July, 21
Sergey Malinke,22 mwenye asili ya Urusi naye pia alihusishwa na tukio hilo na mwishowe akaachwa huru kama Mshukiwa wa awali.
Polisi wa Ureno walienda kaika chumba cha Madeleine na kufanya uchunguzi wa kisayansi wa kumpata mhusika kwa njia ya DNA yaani Forensic Evidence ila zoezi hilo halikufanikiwa pia kwani hawakupata vinasaba vya mtu yoyote mule chumbani.
Wasamaria wema nchini Uingereza walitangaza kila aina ya zawadi kwa yeyote atakayefanikiwa kumpata binti, mfuko wa kuchangisha fedha wa MADELEINE McCANN FUND; LEAVING NO STONE UNTURNED ulianzishwa ili uweze kuchochea watu wasaidiane katika kumsaka Malaika huyo wa Mungu. Jitihada za kumpata Madeleine hazijafanikiwa kuzaa matunda hadi hivi sasa.

                              Mungu amlinde Madeleine McCann popote pale alipo, Amina

Sunday, May 15, 2011

TRIBUTE TO THE DISAPPEARANCE OF A BRITON MADELEINE McCANN, 4-UEROS

Mamake Kate McCann akilia huku ameshika mdoli wa bintiye Madeleine McCann.
Wazazi wake Madeleine Kate na Gerry McCann wakiwa wamewabeba wadogo zake mapacha Sean na Amelie.
Mtoto Madeleine McCann,4 aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha katika Hoteli ya Praia Da Luz huko Ureno alipokuwa katika mapumziko ya kiangazi yeye pamoja na wazazi wake Kate na Gerry McCann. Jitihada za kumpata zimegonga mwamba hadi hii leo maskini. Nani anamshikilia mtoto huyu asiyejua rangi yoyote Duniani maskini

Wednesday, May 11, 2011

KUMBUKUMBU ZA BOB MARLEY

Marehemu Bob Marley akicharaza gitaa.
Ni mwaka wa 30 tangu Gwiji, mpiganiaji haki na mwanamuziki wa Reggae Bob Marley alipoaga dunia tarehe 11, may, 1981 katika hospitali ya Cedars Lebanon, Miami, Florida, Marekani.

Bob alikuwa mpiga gitaa la ridhimu na muimbaji kiongozi wa bendi za Ska, Rocksteady, Reggae na hatimaye The Wailers (1963-1981), alihamasishwa kuimba  na masuala ya jamii yake katika nchi ya jamaika, kisiasa na kiutamaduni, nyimbo zake kali kama "I shot the Sheriff", "No woman no cry" "Could you be loved" "Jammin na Sti it up" katika albamu alizofanya na kundi la The Wailers za "Buffalo Soldies na Iron Lion Zion". Miaka mitatu baadaye baada ya kifo chake albamu  ya "The Legend'" ilitolewa na kuwa albamu iilouza zaidi ya nakala milioni 25 na kufikia hadhi ya Platinum (Diamond) huko nchini Marekani

Bob Marley alizaliwa kama Nesta Robert Marley katika kijiji cha Nine Mile huko St. Ann Parish na Baba yake Mzee Narval Sinclair Marley ambaye alikuwa mjamaika- mzungu mwenye lafidhi ya Uingereza ambaye familia yake ilitokea Essex, Uingereza na nahodha wa meli ambaye alikuja kumuoa mjamaika-mwafrika Codella Booker aliyekuwa na umri wa miaka 18, walijitahidi kuea familia yao japokuwa Babake Bob muda mwingi alikuwa safarini ambapo mwaka 1955 Bob akiwa na miaka 10 Babake alifariki kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo(Heart attack) akiwa na miaka 60, alipooulizwa kuhusu asili yake Bob alijibu kuwa

            "I dont have prejudice against meself. My father was a white and my mother was black, then call me half-caste or whatever. Me dont dip on nobody's side. Me dont dip on the black man's side nor the white man's side. Me dip on God's side, the one who create me and cause me to come from black and white"

Alipokuwa katika ziara zake za Ulaya , Bob alipata kudhuru kidole chake alipokuwa akicheza mpira wa miguu huko jijini Paris,Ufaransa mwaka 1977 alikutwa na kansa aina ya Acral Lentiginon Melanoma aina ya  Malignant melanoma. Baadaye alirudi Marekani ambapo alifanya maonyesho mawili (Gigs) katika ukumbi wa Madison Square Garden jijini New York huku akijua kuwa kupona yeye ilikuwa haiwezekani maskini. Ugonjwa ulisambaa hadi katika ubongo na hatimaye akapelekwa katika hospitali ya huko Miami ambapo aliaga dunia asubuhi ya May, 11, 1981 na kuzikwa May, 21, mazishi yake yalifanywa kitaifa karibu na mahala alipozaliwa yakihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamaika Edward Seaga ambaye alitoa wasifu ufuatao kwa Marehemu

                "His voice was an omnipresent cry in our electronic world. His sharp features, majestic looks and prancing style a vivid etching on the landscapes of our minds. Bob Marley was never seen. He was an experience which left an indelible in print with each encounter. Such a man can not be erased from the mind. He is part of the collective consciousness of the nation"

alihitimisha Waziri katika msiba wa kinara huyu aliyepigania uhuru, haki na usawa wa watu weusi kupitia nyimbo zake. Mungu amrehemu.....

Thursday, May 5, 2011

OSAMA- KILA BINADAMU ANA MWISHOWE

    Marehem Osama bin Laden a.k.a Obama bin Laden aliuawa huko Abbottabad mnamo May, 2, 2011, mjini Islamabad, Pakistan na majasusi wa marekani. Alivamiwa nyumbani kwake majira ya saa 2 asb ndipo katika purukushani za kutaka kujiokoa aliishia kupigwa shaba ya kichwa na kuaga dunia papo hapo, picha za maiti yake hazijaoneshwa mpaka sasa kwa mintaarafu ya kiusalama, Marekani imeamua kufanya hivyo kuhofia kupandikiza chuki na hasira zaidi kwa wafuasi wake ambao huenda wakataka kulipiza kisasi kutokana na ubaya watakaouona kutoka katika picha hizo. Osama ambaye maiti yake inasemekana imezikwa chini ya bahari ya Arabu ya kaskazini, kitendo ambacho kimezusha maswali mengi kwa watu mbalimbali kuwa je, ni sahihi? Naye Sheikh Abdul Basaleh kutoka Tanzania alijibu kuwa binadamu yeyote aweza zikiwa baharini endapo tu atafia humo, pili, ikiwa labda kuna hofu ya kuharibika kwa maiti yake pia kwaweza sababisha maziko yake yakawa baharini.
     Hakuna mtu wa kukataa wala kukubali kuwa Mzee huyu aliwanyima sana usingizi Wamarekani kwa zaidi ya muongo, watu walikuwa wakiiishi kwa hofu na wahaka sana kwa sababu yake maskini, hasa baada ya mashambulizi yake katika kituo cha biashara duniani World Trade Centre jijini New York na Kambi za Pentagon katika mji wa Washington ambayo yalipoteza maisha ya watu zaidi ya 3000, miaka 3 kabla alihusishwa pia na milipuko ya mabomu katika Balozi za Marekani mjini Dar-es-Salaam na Nairobi ambapo zaidi ya watu 200 walihofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa, na shambulizi hili ambalo liliendana na oparesheni kali dhidi ya ugaidi na hatimaye kukamatwa kwa baadhi ya washukiwa wa kitanzania ambaye mmojawapo ni Mzanzibar Mohammed Ghailani ambaye alipatikana na hatia na hatimaye kuhukumiwa kifungo cha maisha Marekani miezi kadhaa mwaka huu maskini, Mohammed angali kijana 23 atasotea maisha yake yote gerezani.
      Mmoja wa wachambuzi wa siasa za ulimwengu  Suleman Salum alihoji sana kuhusu kifo cha Osama kwa kudai kuwa hata wamarekani ni magaidi kwa namna walivyomuua Osama kwa sababu alipaswa akamatwe apelekwe Mahakamani akatoe sababu kwa nini alikuwa akifanya vitendo hivyo viovu kama cha September 11? lakini kitendo cha wao kumuua kimedhihishia ulimwengu uchakaramu na umuflis wao, lakini pia opereshani za kumsaka mtu huyu pia zilikuwa za kigaidi kwa kuvamia nchi za  Afghanistan, Iraq na kuanza kuteketeza mamia ya watu ya watu ambao hawana hatia hata chembe, Salum aliiambia Idhaa ya Kiswahili ya BBC.
      HOJA KUNTU;
     Kumekuwa na kasumba ya watu walio na majina ya kiislamu kubaguliwa sana pindi watakapo kusafiri kwenda nchi mbalimbali za Maghreb kama Marekani na Uingereza kwa kuwanyima viza na hata vibali vya kuishi katika nchi hizo kwa ajili ya majina yao, hivi ni kweli jina huweza sadifu itikadi, hulka na mwenendo mzuri au mbaya wa mtu jamani kama si ubaguzi wangapi washafanya matukioya ajabu ilhali si waislamu kama Coperland aliyekuwa akiwaua watu weusi kule kitongocha Brixton kusini mwa London, Uingereza huyu naye ni muislam na ana jina la kiislam kama Osama? Rais wa Marekani Barack Obama amedai kuwa suala la Ugaidi halihusishwi na dini yoyote bali imani za mtu tu, huwezi kumnyooshea mtu kidole kuwa ni gaidi kwa kuwa ni mwislam au mkristo, la hasha, alidai Mjaluo Obama.
      
Marehemu Osama bin Laden akiwa na Mwandishi wa Habari Hamid Amir mwaka 1997
     Osama bin Mohammed bin Awad bin Laden alizaliwa Machi 10, 1957 huko Riyadh, Saudi Arabia alikuwa muumini wa dhehebu la wahabi na alipenda sana kusoma Quran na kufanya jihad, Wazazi wake waliachana angali mdogo bado na kulelewa na Baba wa Kufikia ambapo walizaliwa ndugu zake wengine wanne, alisoma Uchumi na Utawala wa baishara katika Chuo Kikuu cha  King Abdulaziz mwaka 1981 huko Saudia. Alioa mara nne na kuzaa watoto 25-26.
     Marehem Osama aliamini kuwa Sharia Law ndo suluhisho la matatizo yote ulimwenguni...
                                                             R.I.P